Siku ya Wanawake Duniani husherekewa Machi 8 kila mwaka,Rais wa Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (VoWET) Maida Waziri na Mkurugenzi wa IBRA Contractors amewataka wanawake nchini kujituma na kuwa wabunifu katika biashara zao jambo litakalo wapelekea kufanikiwa, huku akisisitiza elimu na mtaji siyo chanzo cha kukata tamaa bali kufanya kazi kwa bidii na kutumia taarifa sahihi zitakazo wapelekea kufanukiwa kama ilivyokuwa kwake, ambaye amefikia hatua ya kupewa tuzo na Rais Mstaafu Jakaya Kikwetu kwa kuwa Mkandarasi bora 2011-2015.
Kauli mbiu yetu TANZANIA YA VIWANDA INAWEZEKANA TUWEZESHWE MAZINGIRA RAFIKI YA KODI
Rais wa Vowet akibebwa juu kwa furaha baada ya kumaliza hotuba yake.